RESEARCH AD

RESEARCH AD

CLEARING AND FORWADING

CLEARING AND FORWADING

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

THE GUARDIAN LTD

Habari Picha

ZITTO KABWE : UBUNGE SASA BASI!

Zitto Kabwe na Joseph Mbilinyi
Na: Frank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma, MWANANCHI.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

 “Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.

 “Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu. “Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.” Atangaza kugombea urais Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. “Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea. 

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”

 “Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46. Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa. 

 “Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

 “CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto. Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.
 Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari
MAMBA MZITO ZAIDI MAREKANI ANASWA

Mamba aliyekamatwa Mississippi

MAMBA mwenye uzito wa kg. 316 amenaswa kufuatia juhudi ya kumsaka iliyofanywa na watu wanne kwenye ranchi ya Mississippi nchini Marekani na ameweka rekodi ya kuwa mamba mzito zaidi nchini humo.

Eneo la chini la Mississippi Delta linahusisha klabu nyingi za uwindaji, ardhi ya mbao, kilimo na maeneo ya hifadhi za wanyama.

Rekodi ya awali nchini humo ilikuwa ni mamba mwenye uzito wa kg. 312 na alikamatwa mwaka jana kwenye maji hayo hayo ya Delta.

Mamba huyo ana urefu wa futi 13 na inchi 1.5.

Hata hivyo, rekodi rasmi za mamba wakubwa zaidi duniani zinashikiliwa na mamba wawili wenye urefu wa futi 20 (mita 6.2) na kg 1,200.

Mamba wa kwanza aliuawa Mto Mary kaskazini mwa Australia mwaka 1974 na kupimwa na maafisa wa wanyama. Mamba wa pili aliuawa mwaka 1983 katika Mto Fly, Papua New Guinea. Katika suala la mamba wa pili, kilichopimwa kilikuwa ni ngozi ya mamba huyo na inafahamika kwamba ngozi pekee huwa inatoa vipimo pungufu vya urefu halisi wa mnyama, hivyo mambo huyo inawezkana alikuwa na urefu wa sentimeta 10 zaidi.
LEMA AFURAHIA KESI YAKE KUSIKILIZWA NA JAJI MKUU

Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Othman Chande
Godbless Lema
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa anaamini Mahakama ya Rufaa itapitia vyema vipengele vya kesi iliyompoka ubunge wake na kutoa uamuzi wa haki kwavile anamuamini Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande.

Akizungumza katika mahojiano yake leo na kituo cha redio cha Clouds FM kupitia kipindi cha Bongo Amplifanya, Lema amesema kuwa yeye binafsi hataki kupendelewa bali haki itendeke na kwamba anaamini kuwa uamuzi wa jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa litakaloongozwa na Jaji Chande utakuwa ni wa haki na yuko tayari kuupokea.

"Sitaki upendeleo, nipendelewa nitaogopa, nitalia... niko tayari  kurudi kwenye uchaguzi, na ninaamini nitashinda kwa idadi ya kura za kubebwa kwenye canter.... nimefurahi kuwa kesi hii itaongozwa na Jaji Mkuu Chande," amesema.

'Yeye (Chande) ndiyo mkuu wa mahakama... ninaamini vipengele vitapitiwa kwa haki," amesema Lema ambaye ubunge wake ulitenguliwa na mahakama kutokana na kasoro kadhaa na hivyo akakata rufaa kupinga uamuzi huo
 MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA

Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema akihutubia

Mhe. Lema akiwa na Mhe. Joshua Nassari

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe.Joshua Nassari akihutubia

Kada aliyejitoa CCM Arusha Ally Bananga


KIKAO CHA NEC YA CCM KINACHOENDELEA DODOMA 


 


JK ASEMA ANAYETAKA KUONDOKA CCM RUKSA

NI WALE WANAOTISHIA BAADA YA KUTOSWA, AWASHANGAA WANAOTISHIANA SILAHA KWA AJILI YA UONGOZI

   Na: Midraji Ibrahim na Habel Chidawali, Mwananchi  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewatolea uvivu wagombea wa nafasi mbalimbali ambao majina yao yamekatwa, akisema wanaotaka kukihama chama hicho kwa sababu wametoswa, waondoke haraka. Licha ya kuwatakia safari njema, Rais Kikwete aliwatupia lawama baadhi ya wanaCCM ambao wameripotiwa kuendesha malumbano na kugeuza uchaguzi huo kama uwanja wa vita. Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) jana, Rais Kikwete alisema kumekuwapo na taarifa mbalimbali ambazo zimemfikia pia kwamba baadhi ya wanachama wanatishia kukihama chama hicho kama majina yao yatakatwa.  “Wako wenye ndimi mbili ambao wanasema kuwa wasipoteuliwa wanaweza kuondoka. Ah! Mimi nasema watangulie huko maana inaonyesha kuwa walishaandaa maeneo ya kwenda,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wajumbe wa Nec. Alisema CCM kinayo taarifa kuhusu watu kugombana na hata kutoleana silaha, jambo alilosema linashangaza, huku akihoji kuna nini katika uongozi tena Nec? “Uchaguzi usigeuzwe uwanja wa fujo. 

Wengine wanatoleana silaha kama majembe, ngumi na silaha nyingine, hivi wanagombana nini huko? Uchaguzi usigeuzwe kuwa ni uwanja wa vita.” alisema. Hivi karibuni, baadhi ya makada wa chama hicho wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kukitishia chama hicho akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye alikaririwa akisema kama jina lake halitapitishwa, patachimbika. Mbunge huyo alisema hayo siku chache baada ya jina lake kutupwa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi iliyokuwa ikipitia na kuteua wagombea watatu kwa ajili ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo. 


"Hapatatosha CCM," alisema Mkono alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoswa kwake katika mchujo wa awamu hiyo ya awali. Ingawa Rais Kikwete hakutaja majina, Mbunge wa Nzega Dk Khamis Kigwangallah na Hussein Bashe nao waliripotiwa kutoleana maneno makali hata kuonyeshana bastola, huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na Mbunge wa Kahama, James Lembeli wakiendesha malumbano kwa muda mrefu. Inadaiwa kuwa majina hayo yote na ya vigogo wengine yamekatwa na jana baadhi yao walikuwa wanadai kuwa CCM kinataka kuzalisha upinzani ambao utakisababishia kushindwa katika safari yake kisiasa hasa katika mfumo huu wa vyama vingi. Licha ya makaripio hayo, Rais Kikwete alibainisha kuwa CCM kinasemwa na watu kuwa kinakithiri rushwa katika chaguzi zake hivyo akawataka wagombea kubadilika kabla ya kukamatwa na Takukuru. “Zipo taarifa ingawa hatujazithibitisha kwamba wapo baadhi ya wagombea wanamwaga fedha sijawahi kuona… Takukuru wapo wanaendelea na kazi. Chama chetu kinasemwa tujipe fursa ya kubadilika, tusisubiri kukamatwa na kuanza kuilaumu PCCB.” 


Kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, Rais Kikwete alisema katika uchaguzi huo, wamejitokeza watu wengi tena vijana wasomi na kwamba Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu, zimewapandisha na kuwakata waliotumikia chama muda mrefu. “Kama hukuteuliwa kuna mawili, ama nafasi zimejaa au hufai una upungufu kidogo na huo ni utaratibu wa chama siyo kuoneana,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa. 


Alisema katika uteuzi huo vijana watapewa nafasi zaidi kutokana na ukweli kuwa, chama bila ya vijana hakiwezi kuwa imara kwa sababu ndiyo nguvu ya ushindi. “Hao watakaoachwa watambue kuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza timu ya ushindi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa Bara na Visiwani, hivyo kuachwa jina lako isiwe nongwa,” alisema na kuongeza: “Lazima tukipe chama chetu watu wa kushinda… Lazima tutambue sasa tunaunda timu ya ushindi wa chama siyo ushindi wa mtu.” Hata hivyo, Rais Kikwete alitoa angalizo kuwa anajua kikao cha Halmashauri Kuu kingekuwa na mjadala mzito, lakini lazima wakipe chama watu wa kushinda. Majina manne Kamati Kuu ya CCM, inadaiwa kupendekeza majina ya wagombea wanne kwenye jumuiya zake, tofauti na kanuni ya chama hicho ya nafasi moja kuwaniwa na watu watatu. Kikao chake kilichomalizika juzi usiku, kinadaiwa kubadili kanuni ya kupendekeza wagombea watatu kwa nafasi moja na kwamba, hivi sasa mapendekezo hasa kwenye jumuiya ni wagombea wanne. 

 Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa, hatua hiyo inalenga kutoa ushindani kwa wagombea. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipotakiwa kuzungumzia suala hilo hakukanusha wala kukubali zaidi ya kusema kwamba hata kama utaratibu huo umetumika siyo mara ya kwanza kwa chama hicho. Alisema kama Jumuiya ya Vijana wanaojitokeza lengo lao linakuwa kupata uzoefu na kwamba, idadi ya majina inategemeana na busara za kikao kinavyoona ili kutoa nafasi kwa wagombea kujipima. Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz
UJENZI WA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI UNAVYOENDELEA ENEO LA KIMARA-MWISHO JIJINI DAR ES SALAAM LEO SEPT 26, 2012





CHADEMA KATIKA KESI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA ARUSHA MJINI Mh GODBLESS LEMA

Gari ya polisi ikiwa imepaki pembeni kupisha maandamano ya wafuasi wa CHADEMA
Wafuasi wa CHADEMA wakielekea katika ofisi za chama



Msafara wa wafuasi wa CHADEMA wakitokea mahakamani kuelekea ofisi za chama hicho




Gari alilopanda aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA)Godbless Lema likiwa linasukumwa na wafuasi wa chama hicho mara baada ya kutoka mahakamani
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Mh Godbless Lema akiongea na wananchi nje ya ofisi ya chama mara baada ya kutoka mahakamani
Wananchi wakiwa nje ya ofisi ya CHADEMA wanamsikiliza aliyekua mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless lema


RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI


Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Kigamboni katika hafla iliyofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk Ramadhani Dau. NSSF itagharamia asilimia 60 za ujenzi wa daraja hilo na serikali asilimia 40. Picha na Freddy Maro-IKULU


UJENZI UNAVYOENDELEA BARABARA YA MOROGORO (MOROGORO ROAD) ENEO LA KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM







BARAZA LA VIJANA CHADEMA(BAVICHA) TAIFA WAKUTANA MOROGORO KWA AJILI YA KUWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA CHAMA
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakipitia ajenda za kikao
Wajumbe wakisimama kwa muda mfupi kuwakumbuka waliopoteza maisha
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche akifungua kikao
Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa zamani wa TBC, Jerry Muro ( kushoto) akito salamu zake kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji cha Bavicha Taifa iliyoketi Mjini Morogoro kuanzia Septemba 14 hadi 18, mwaka huu.

KWA HABARI HII YA UTABIRI WA HALI YA HEWA (MVUA INAYOTARAJIWA KUNYESHA KARIBUNI),SIJUI DAR ES SALAAM ITAKUWAJE MAENEO YA MABONDENI KAMA HAYA!
HAPA NI ENEO LA KIMARA MWISHO JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AZINDUA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA,KUNDUCHI JIJINI DA ES SALAAM
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala leo Septemba 10, 2012 baada ya kumkabidhi mfano wa funguo kama ishara ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makakala (katikati), wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wageni mbalimbali waalikwa pamoja na Balozi  na Maofisa wa Ubalozi wa China waliopo nchini, wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho, Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makakala, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho, cha Ulinzi cha Taifa, Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wageni mbalimbali waalikwa pamoja na Balozi  na Maofisa wa Ubalozi wa China waliopo nchini, wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho pamoja na kozi ya kwanza ya chuo, Kunduchi, jijini Dar es Salaam leo.

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Emmanuel Nchimbi, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati alipokuwa akikizindua Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya wanafunzi wa kwanza wa Chuo hicho, wakitoa heshima zao kwa Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi huo leo.

Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Meja Jenerali Charles Makakala, akimueleza jambo Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kukizindua Chuo hicho cha Ulinzi cha Taifa na kozi ya kwanza ya chuo leo. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange. 


 Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa na baadhi ya wanafunzi wa kwanza wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, mara baada ya kukizindua, Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa katika uzinduzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwenye uzinduzi wa chuo hicho.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma akipozi na wanachuo wa kozi ya kwanza ya bmwaka mmoja katika Chuo cha UIinzi (National Defence College) alichofungua rasmi leo Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU

MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI DAR LEO





PICHA ZA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI  UNAOENDELEA BARABARA YA MOROGORO (MOROGORO ROAD) KATIKA ENEO LA KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM















No comments: